Majadiliano haya yamelengwa ili kuwawezesha vijana kupata taarifa za kina juu ya Nishati na Mabadiliko ya Tabia Nchi, kujadili masuala muhimu yanazunguka Nishati na Tabia Nchi duniani kote. Mkutano huo pia una lengo la kuchangia kwenye mijadala inayoendelea ya Ajenda za baada ya 2015 ya Dunia tunayoitaka.
Tangu mwaka 2006 Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa ya Tanzania, Asasi ya Umoja wa Mataifa ya Kenya, Asasi ya Umoja wa Mataifa ya Uganda, tumekua tukiandaa Baraza Kuu Kivuli La Kimataifa la Kanda ya Afrika Mashariki kwa ajili ya vijana kila mwaka. Mikutano hii huwa ina lengo kuu la kushirikisha vijana katika majadiliano ya Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia.
Mkutano wa mwaka huu imekuwa kufadhiliwa na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje; Ubalozi wa Norway; Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa;. Tunatumia fursa hii kuwaomba vijana wote wa Afrika ya Mashariki pamoja na jamii kujiunga na vijana wanapokutana katika majadiliano haya ya Malengo ya Maendeleo ya Kimilenia. Pia tunachukua nafasi hii kuwaomba mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali kuungana mikono na vijana wanaposhiriki katika fursa hii pekee inayolenga kuleta vijana wa Tanzania karibu zaidi na Umoja wa Mataifa na vilevile kwa ulimwengu.
0 comments:
Post a Comment